Dosari Za Kifonolojia Zinazojidhirisha Miongoni Mwa Wajifunzaji Wa Kiswahili Katika Jamii Ya Wachiga: Uzingativu Wa Muktadha Wa Kujifunzia.

Utafiti huu unahusu dosari za kifonolojia zinazojitokeza miongoni mwa wajifunzaji wa Kiswahili katika jamii ya Kichiga. Lengo lilikuwa kutalii ili kuona muktadha wa kijamii unavyoukilia ujitokezaji wa dosari hizo za kifonolojia. Kwa mahsusi kabisa, utafiti huu ulilenga kubainisha dosari za kifonoloj...

Full description

Saved in:
Bibliographic Details
Main Author: Turigye, Rosemary
Format: Thesis
Language:English
Published: Kabale University 2025
Subjects:
Online Access:http://hdl.handle.net/20.500.12493/2881
Tags: Add Tag
No Tags, Be the first to tag this record!
Description
Summary:Utafiti huu unahusu dosari za kifonolojia zinazojitokeza miongoni mwa wajifunzaji wa Kiswahili katika jamii ya Kichiga. Lengo lilikuwa kutalii ili kuona muktadha wa kijamii unavyoukilia ujitokezaji wa dosari hizo za kifonolojia. Kwa mahsusi kabisa, utafiti huu ulilenga kubainisha dosari za kifonolojia, kuelewa chanzo chake, kuzingatia muktadha wa kujifunza, na kutoa mapendekezo ya mikakati inayoweza kutumika kupunguza dosari hizo. Utafiti ulitumia sampuli ya watoa taarifa 94 waliogawanyika katika sehemu mbili, walimu 10 na wanafunzi 84. Mbinu za kukusanya data zilizotumika ni uandishi wa insha na hojaji. Hojaji zilitumika kwa walimu na wanafunzi wakati uandishi ulitumika kwa wajifunzaji lugha. Utafiti uliongozwa na Nadharia Uchanganuzi Makosa na Nadharia Elekezi hasa kwa mahsusi wake muhimili wa ingizo. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa dosari za udondoshaji, uchopekaji na ubadilishaji wa sauti zilibainika. Utafiti umebaini kuwa chanzo cha dosari hizo ni pamoja na uhamishaji, athari za lugha ya Kichiga, utamaduni wa Kichiga na ukakamaaji. Vilevile, imebainika kwamba, muktadha wa kijamii unachochea kwa kiasi kikubwa uibuzi wa dosari za kifonolojia kutokana na ukosefu wa uibuzi wa ingizo ndani ya mazingira miongoni mwa wajifunzaji wa lugha ya Kiswahili katika jamii. Muktadha wa kujifunzia uligunduliwa kuwa una athari kubwa kwa ujitokezaji wa dosari za kifonolojia, kwani wajifunzaji walikuwa wakipata changamoto kutokana na ukosefu wa mazoezi na matumizi ya lugha ya Kiswahili katika mazingira yao ya kila siku. Aidha, mikakati anuwai ilipendekezwa ili kupunguza dosari za kifonolojia, kuongeza mazoezi ya kusikiliza na kuzungumza Kiswahili, kuboresha vifaa vya kufundishia na kujifunzia, na kuanzisha programu za msaada kwa wajifunzaji wenye dosari za kifonolojia. Kwa kufanya hivyo, inatarajiwa kuwa dosari za kifonolojia zinaweza kupunguzwa na ujuzi wa lugha ya Kiswahili unaweza kuboreshwa miongoni mwa wajifunzaji katika jamii ya Kichiga.