Uvulivuli wa Tafsriri kutoka Lugha za Asili kwenda Lugha ya Kiswahili Mfano wa Albamu ya Kikinga ya Sumasesu Theatre Art Group.

Katika taaluma ya tafsiri, uvulivuli wa matini zilizotafsiriwa umejikita zaidi kwenye tafsiri za lugha za kigeni kwenda lugha za asili au lugha za asili kwenda lugha za kigeni. Mathalani tafsiri ya Kiingereza kwenda Kiswahili ama Kiswahili kwenda Kiingereza (Maro, 2018). Chukulia94 ikiwa ni kwamba u...

Full description

Saved in:
Bibliographic Details
Main Author: Msigwa, Arnold B. G.
Format: Article
Language:English
Published: Kabale University 2024
Subjects:
Online Access:http://hdl.handle.net/20.500.12493/2390
Tags: Add Tag
No Tags, Be the first to tag this record!
Description
Summary:Katika taaluma ya tafsiri, uvulivuli wa matini zilizotafsiriwa umejikita zaidi kwenye tafsiri za lugha za kigeni kwenda lugha za asili au lugha za asili kwenda lugha za kigeni. Mathalani tafsiri ya Kiingereza kwenda Kiswahili ama Kiswahili kwenda Kiingereza (Maro, 2018). Chukulia94 ikiwa ni kwamba uvulivuli huo unatokana na wafasiri kutokuwa na umilisi wa lugha za kigeni hasa Kiingereza, na ama tofauti za kiutamaduni baina ya lugha mbili; yaani matini chanzi na matini lengwa. Jitihada kidogo zimejishughulisha na uvulivuli wa tafsiri zilizotafsiriwa kutoka lugha za asili kwenda Kiswahili na athari zake kimawasiliano. Utafiti huu ulichunguza Uvulivuli wa Tafsiri kutoka lugha ya Kikinga kwenda lugha ya Kiswahili mfano Albamu ya Sumasesu Theatre Art Group. Sampuli ya utafiti huu ni nyimbo tano za Albamu ya Sumasesu Theatre Art Group. Usampulishaji tabakishi ndiyo ulitumika kupata nyimbo hizo. Data zilikusanywa kwa njia ya uchanganuzi matini, ambapo nyimbo zilisikilizwa mara tatu, kisha kudondoa tafsiri iliyotolewa kutoka lugha ya Kikinga kwenda Kiswahili zenye uvulivuli kwa kuzingatia kaida za lugha ya Kikinga. Makala haya yaliongozwa na Nadharia ya Usawe wa Kidhima (Nida, 1964) na kuendelezwa na Nida & Tiber, (1969). Data zilichanganuliwa kwa njia ya maudhui na kuwasilishwa kwa njia ya majedwali na ufafanuzu kutolewa kwa njia ya maelezo. Matokeo ya utafiti huuyameonesha kuwa kuna utumiaji wa visawe vya lugha ya Kiswahili ambavyo si sahihi katika tafsiri iliyotolewa kiasi cha kuhamisha maana ya msingi ya matini chanzi. Mathalani, maana ya msingi ikibatilishwa, ujumbe uliolengwa katika matini chanzi unaathiriwa na hivyo kumfanya msikilizaji wa matini lengwa kutopata athari iliyolengwa na msanii. Kutokana na uvulivuli huo, makala yanapendekeza utafiti mwingine na mpana zaidi kufanyika kuhusu tafsiri za kutoka lugha za asili kwenda lugha ya Kiswahili kutumia data pana zaidi. Utafiti kama huo ukifanyika unaweza kubadili mtazamo wa wana nadharia kwamba, uvulivuli wa tafsiri ni tokeo la wafasiri kutojua lugha wanazozishughulikia au tofauti za kiisimu kati ya lugha chanzi na lugha lengwa; kwa sababu kiisimu Kikinga na Kiswahili zote ni lugha za Kibantu na pia waliofasiri nyimbo hizo ni wazawa wa Kikinga na ambao sio wazawa wa Kiswahili.