Mchango Wa Methali Za Kiswahili Katika Kukuza Umilisi Wa Lugha Ya Kiswahili Kwa Wanafunzi Wa Shule Za Upili Wilayani Ntungamo.

Mada ya utafiti huu ilikuwa ni Mchango wa Methali za Kiswahili katika Kukuza Umilisi wa Lugha ya Kiswahili kwa Wanafunzi wa shule za Upili Wilayani Ntungamo. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza mchango wa methali za Kiswahili katika kukuza umilisi wa lugha ya Kiswahili kwa wanafunzi wa s...

Full description

Saved in:
Bibliographic Details
Main Author: Katsigaire, Joshua
Format: Thesis
Language:en_US
Published: Kabale University 2024
Subjects:
Online Access:http://hdl.handle.net/20.500.12493/2106
Tags: Add Tag
No Tags, Be the first to tag this record!
Description
Summary:Mada ya utafiti huu ilikuwa ni Mchango wa Methali za Kiswahili katika Kukuza Umilisi wa Lugha ya Kiswahili kwa Wanafunzi wa shule za Upili Wilayani Ntungamo. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza mchango wa methali za Kiswahili katika kukuza umilisi wa lugha ya Kiswahili kwa wanafunzi wa shule za upili wilayani Ntungamo. Kwa kutumia njia ya Mahojiano mtafiti alipata data za lengo la kwanza na za lengo la pili,sampuli iliyotumiwa ni shule za upili nne (4) na wanafunzi arobaini (40) wa kidato cha tatu wanaosoma lugha ya Kiswahili, ili kupata lengo la kwanza na la pili,methali mbali mbali za Kiswahili zinanokuza umilisi wa lugha zilikusanywa halafu na kuchunguzwa ili kupata ujumbe uliyomo kwa hali ya kutimiza lengo la pili la kufafanua ujumbe uliyomo katika methali za Kiswahili zinzofundishwa kwa wanafunzi wa shule za upili wilayani Ntungamo. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kwamba zipo methali nyingi za Kiswahili ambazo huchangia katika kukuza umilisi wa wamafunzi wa lugha ya Kiswahili na methali hizo wanafunzi wanazijua tuu kimuundo lakini kifasihi hawazielewi kwa mfano,Mwacha asili ni mtumwa,Aliye juu mngoje chini,na Kidole kimoja hakivunji chawa. Pia matokeo ya methali yanaonyesha kwamba katika shule za upili Maanisipa ya Ntungamo, walimu wa Kiswahili wanajaribu kuwafunza wanafunzi wa kidato cha pili methali za Kiswahili ili wapate ujumbe uliyomo kwa ajili ya kutimiza lengo la pili. Utatiti huu ulikuwa ni wa kiwango cha shahada ya awali, ulichunguza methali chache tu kutoka shule za upili wilayani Ntungamo. Methali zilizokusanywa zinaakasi umulisi wa lugha ya Kiswahili. Utafiti mwingine wa kina kiwango cha Umahiri unapendekezwa kufanywa ili kupata michango mbali mbali nyingine ya methali za Kiswahili zinazokuza umilisi wa lugha ya Kiswahili .Ni imani yetu kwamba, tulichokipata uwandani kinaweza kuwa ni fununu tu juu ya mambo mengi yalifichama katika methali za Kiswahili. Utafiti huu unapendekezwa kwa kiwango cha shahada ya umahiri, unaweza kufanywa ili kupata michango mbali mbali nyingine ya methali za Kiswahili zinazokuza umilisi wa Lugha ya Kiswahili.