Nafasi ya Leksikoni yenye Vipashio Ghairi kutoka Kiingereza na Kiarabu katika Fonolojia ya Leksikoni ya Kiswahili Sanifu
Makala haya yanahusu ubainishaji wa nafasi ya leksikoni ya mkopo yenye vipashio ghairi katika leksikoni ya Kiswahili sanifu. Data zilizotumiwa katika makala haya zilikusanywa kutoka makavazi ya Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mbinu za uhakiki matini na usomaji nyaraka...
Saved in:
Main Author: | |
---|---|
Format: | Article |
Language: | English |
Published: |
2023
|
Online Access: | http://hdl.handle.net/20.500.12493/1138 |
Tags: |
Add Tag
No Tags, Be the first to tag this record!
|
Summary: | Makala haya yanahusu ubainishaji wa nafasi ya leksikoni ya mkopo yenye vipashio
ghairi katika leksikoni ya Kiswahili sanifu. Data zilizotumiwa katika makala haya
zilikusanywa kutoka makavazi ya Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam. Mbinu za uhakiki matini na usomaji nyaraka zilitumiwa
kukusanya data. Uhusiano wa matabaka ya leksikoni ya Kiswahili umeelezwa kwa
kutumia modeli ya uhusiano wa KIINI-PEMBEZONI ya Itô na Mester (1995)
sambamba na Nadharia ya Umbo Upeo (UU). Data imedhihirisha kuwa leksikoni
ya Kiswahili inatoa ushahidi kuwa kuna matabaka mbalimbali ndani yake. Modeli
iliyotumiwa imetuwezesha kubainisha mwingiliano taratibu na utabakishi wa
leksikoni ya Kiswahili. Leksikoni ya Kiswahili yenye viambajengo ghairi husika
imetambuliwa kisinkronia kwa kuwa viambajengo hivyo vina mchango katika
sarufi ya Kiswahili (fonolojia ya leksikoni ya Kiswahili) hasa kuhusiana na
mashartizuizi ya kimuundo. Matokeo yamebainisha kuwa mashartizuizi ya
leksikoni ya Kiswahili iliyopokelewa kutoka Kiingereza na Kiarabu na
viambajengo ghairi yanafanya kazi katika mawanda ya PEMBEZONI. |
---|