Mradi wa Kuandika Tamthilia ya "Kiza Cha Mchana''.

Mradi huu wa tamthilia umepewa anwani ya " kiza cha mchana " kimaksudi. K wa kawaida kiza hujitokeza wakati wa usiku lakini siyo wakati wa mchana kwa hivyo kiza kikijitokeza mchana kuna maana kwamba kuna kitu ambacho hakiko sawa. Mtu yeyote azaliwapo huwa anatarajia mema na ufanisi katika...

Full description

Saved in:
Bibliographic Details
Main Author: Masika, Doreen
Format: Thesis
Language:en_US
Published: Kabale University 2023
Subjects:
Online Access:http://hdl.handle.net/20.500.12493/1072
Tags: Add Tag
No Tags, Be the first to tag this record!
_version_ 1803933480285896704
author Masika, Doreen
author_facet Masika, Doreen
author_sort Masika, Doreen
collection KAB-DR
description Mradi huu wa tamthilia umepewa anwani ya " kiza cha mchana " kimaksudi. K wa kawaida kiza hujitokeza wakati wa usiku lakini siyo wakati wa mchana kwa hivyo kiza kikijitokeza mchana kuna maana kwamba kuna kitu ambacho hakiko sawa. Mtu yeyote azaliwapo huwa anatarajia mema na ufanisi katika maisha yake lakini baadhi ya watu duniani na katika nchi hii, matarajio yao hugeuka ndoto ya mchana yaani huishia yakiwa kinyume kabisa na matarajio ya watu hawa. Mradi wa tamthilia ya "kiza cha mchana" utadhihirisha wazi wazi jinsi baadhi ya watu wanakumbana na matatizo chungu nzima; tatizo baada yajingine mpaka wanapoanza kujichukia na kulaani siku walizozaliwa. Tamthilia hii itamtia mtu moyo ambaye anakumbana na matatizo katika maisha yake kwamba matatizo ni sehemu ya maisha ya binadamu na sio mwisho wa maisha ya binadamu, wakiyavumilia wakaendelea kujitahidi kadri ya uwezo wao huku wakimwomba Rabana, mwishowe watafanikiwa na hali yao kubadilika kabisa na kuanza kuishi kwa raha mustarehe. Mhusika mkuu, Matatizo ambaye ni fakiri atakumbana na matatizo mengi; moja baada ya jingine licha ya kuwa mchochole wa kupigiwa mfano. Matatizo analemewa na kuanza kujichukia na mwishowe anaokoka na baada ya muda mfupi anafanikiwa na kutajirika kutokana na bahati asiyoilalia wala kuiamkia. Watu kama hawa huishia kwa kujitia kitanzi baada ya kukumbana na mfululizo wa matatizo kama njia ya kuondokea matatizo haya na kuiacha familia yao katika dhiki kubwa. Kwa hivyo, mradi huu unapinga kabisa kuj itia kitanzi kama suluhisho la mfululizo wa matatizo bali kuwatia moyo na kuendelea kufukuza ndoto zao huku wakiimezea mate machungu hali yoyote ile wanayokumbana nayo mpaka watakapofaulu. Matatizo hapa amechorwa kama maskini, mvumilivu, ili kuwapa watu kama hawa mfano mzuri. Mradi wa tamthilia utapangwa katika vitendo vitatu na kila kitendo kitakuwa na maonyesho matatu. Kila kitendo kitakuwa na maudhui kuu linalozungumziwa humo ambalo linajitosheleza. Kila onyesho litakuwa na maudhui kuu pamoja na maudhui mengine madogo. Maudhui haya ya vitendo na maonyesho yatachangiana na kukamilishana na kufanya tamthilia nzima yenye wazo kuu la matatizo yaani anwani yenyewe ya mradi. Maudhui yatakayoshughulikiwa yatakuwa miongoni mwa utabaka, matatizo, uasherati, migogoro ya kifamilia, uvumilivu, ukengeushi, unafiki, mabadiliko, dini, baraka. vi Msanii wa mradi atatumia wahusika mbalimbali ambao ni pamoja na wahusika wakuu, wahusika wadogo, wahusika bapa, wahusika mviringo na wahusika wa kisaikolojia. Wahusika hawa watakuwa na mienendo ambayo ni pamoja na wavumilivu, wajibikaji, waaminifu, wakengeushi, washerati, wapole, werevu masomoni, washauri wema. Wahusika wakuu ndio watakaosheheni ujumbe muhimu na wahusika wadogo watawasaidia wahusika wakuu kukamilisha dhamira na maudhui ya msanii. Mazungumzo yataendelezwa miongoni mwa wahusika hawa ambapo nafsi ya kwanza umoja (ni ) na wingi ( tu ) zitatumika hasa kuendeleza mazungumzo baina ya wahusika. Nyimbo, majazi, taswira navyo vitatumika kuwasilisha ujumbe. Wahusika hawa watakuwa na maleba ambayo yataambatana sambamba na mandhari husika na wazo litakalokuwa likiendelezwa na wahusika hawa. Maleba yatakayotumiwa yatakuwa pamoja na magwanda, majoho ya kitabibu, majoho ya mapadre, ndala, veli. Maelekezo ya jukwaa yatatumiwa ipasavyo iii kuwaielekeza hadhira kutambua kwa urahisi maleba, miondoko na maingio ya wahusika na sifa zao. Maelekezo ya jukwaa yataandikwa kwa hati za mkazo na kuwekwa katika mabano. Maelekezo ya jukwaa haya pia yataonyesha wakati na mandhari ambapo vitushi vitatendeka. Mandhari haya yatakuwa pamoja na nyumbani, shambani, zahanatini. hospitalini kanisani.
format Thesis
id oai:idr.kab.ac.ug:20.500.12493-1072
institution KAB-DR
language en_US
publishDate 2023
publisher Kabale University
record_format dspace
spelling oai:idr.kab.ac.ug:20.500.12493-10722024-06-12T07:24:42Z Mradi wa Kuandika Tamthilia ya "Kiza Cha Mchana''. Masika, Doreen Mradi Kuandika Tamthilia Kiza Cha Mchana Mradi huu wa tamthilia umepewa anwani ya " kiza cha mchana " kimaksudi. K wa kawaida kiza hujitokeza wakati wa usiku lakini siyo wakati wa mchana kwa hivyo kiza kikijitokeza mchana kuna maana kwamba kuna kitu ambacho hakiko sawa. Mtu yeyote azaliwapo huwa anatarajia mema na ufanisi katika maisha yake lakini baadhi ya watu duniani na katika nchi hii, matarajio yao hugeuka ndoto ya mchana yaani huishia yakiwa kinyume kabisa na matarajio ya watu hawa. Mradi wa tamthilia ya "kiza cha mchana" utadhihirisha wazi wazi jinsi baadhi ya watu wanakumbana na matatizo chungu nzima; tatizo baada yajingine mpaka wanapoanza kujichukia na kulaani siku walizozaliwa. Tamthilia hii itamtia mtu moyo ambaye anakumbana na matatizo katika maisha yake kwamba matatizo ni sehemu ya maisha ya binadamu na sio mwisho wa maisha ya binadamu, wakiyavumilia wakaendelea kujitahidi kadri ya uwezo wao huku wakimwomba Rabana, mwishowe watafanikiwa na hali yao kubadilika kabisa na kuanza kuishi kwa raha mustarehe. Mhusika mkuu, Matatizo ambaye ni fakiri atakumbana na matatizo mengi; moja baada ya jingine licha ya kuwa mchochole wa kupigiwa mfano. Matatizo analemewa na kuanza kujichukia na mwishowe anaokoka na baada ya muda mfupi anafanikiwa na kutajirika kutokana na bahati asiyoilalia wala kuiamkia. Watu kama hawa huishia kwa kujitia kitanzi baada ya kukumbana na mfululizo wa matatizo kama njia ya kuondokea matatizo haya na kuiacha familia yao katika dhiki kubwa. Kwa hivyo, mradi huu unapinga kabisa kuj itia kitanzi kama suluhisho la mfululizo wa matatizo bali kuwatia moyo na kuendelea kufukuza ndoto zao huku wakiimezea mate machungu hali yoyote ile wanayokumbana nayo mpaka watakapofaulu. Matatizo hapa amechorwa kama maskini, mvumilivu, ili kuwapa watu kama hawa mfano mzuri. Mradi wa tamthilia utapangwa katika vitendo vitatu na kila kitendo kitakuwa na maonyesho matatu. Kila kitendo kitakuwa na maudhui kuu linalozungumziwa humo ambalo linajitosheleza. Kila onyesho litakuwa na maudhui kuu pamoja na maudhui mengine madogo. Maudhui haya ya vitendo na maonyesho yatachangiana na kukamilishana na kufanya tamthilia nzima yenye wazo kuu la matatizo yaani anwani yenyewe ya mradi. Maudhui yatakayoshughulikiwa yatakuwa miongoni mwa utabaka, matatizo, uasherati, migogoro ya kifamilia, uvumilivu, ukengeushi, unafiki, mabadiliko, dini, baraka. vi Msanii wa mradi atatumia wahusika mbalimbali ambao ni pamoja na wahusika wakuu, wahusika wadogo, wahusika bapa, wahusika mviringo na wahusika wa kisaikolojia. Wahusika hawa watakuwa na mienendo ambayo ni pamoja na wavumilivu, wajibikaji, waaminifu, wakengeushi, washerati, wapole, werevu masomoni, washauri wema. Wahusika wakuu ndio watakaosheheni ujumbe muhimu na wahusika wadogo watawasaidia wahusika wakuu kukamilisha dhamira na maudhui ya msanii. Mazungumzo yataendelezwa miongoni mwa wahusika hawa ambapo nafsi ya kwanza umoja (ni ) na wingi ( tu ) zitatumika hasa kuendeleza mazungumzo baina ya wahusika. Nyimbo, majazi, taswira navyo vitatumika kuwasilisha ujumbe. Wahusika hawa watakuwa na maleba ambayo yataambatana sambamba na mandhari husika na wazo litakalokuwa likiendelezwa na wahusika hawa. Maleba yatakayotumiwa yatakuwa pamoja na magwanda, majoho ya kitabibu, majoho ya mapadre, ndala, veli. Maelekezo ya jukwaa yatatumiwa ipasavyo iii kuwaielekeza hadhira kutambua kwa urahisi maleba, miondoko na maingio ya wahusika na sifa zao. Maelekezo ya jukwaa yataandikwa kwa hati za mkazo na kuwekwa katika mabano. Maelekezo ya jukwaa haya pia yataonyesha wakati na mandhari ambapo vitushi vitatendeka. Mandhari haya yatakuwa pamoja na nyumbani, shambani, zahanatini. hospitalini kanisani. 2023-03-06T06:33:31Z 2023-03-06T06:33:31Z 2022 Thesis Masika, Doreen (2022). Mradi wa Kuandika Tamthilia ya "Kiza Cha Mchana''. Kabale:Kabale University. http://hdl.handle.net/20.500.12493/1072 en_US Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/ application/pdf Kabale University
spellingShingle Mradi
Kuandika
Tamthilia
Kiza Cha Mchana
Masika, Doreen
Mradi wa Kuandika Tamthilia ya "Kiza Cha Mchana''.
title Mradi wa Kuandika Tamthilia ya "Kiza Cha Mchana''.
title_full Mradi wa Kuandika Tamthilia ya "Kiza Cha Mchana''.
title_fullStr Mradi wa Kuandika Tamthilia ya "Kiza Cha Mchana''.
title_full_unstemmed Mradi wa Kuandika Tamthilia ya "Kiza Cha Mchana''.
title_short Mradi wa Kuandika Tamthilia ya "Kiza Cha Mchana''.
title_sort mradi wa kuandika tamthilia ya kiza cha mchana
topic Mradi
Kuandika
Tamthilia
Kiza Cha Mchana
url http://hdl.handle.net/20.500.12493/1072
work_keys_str_mv AT masikadoreen mradiwakuandikatamthiliayakizachamchana